Tuesday, 4 August 2009

VAM GENERAL SUPPLY WATIA UBANI MISS EAST AFRICA MORO




Kampuni ya Vam General Supply Co LTD yenye ofisi zake kwenye makutano ya mtaa wa Narung’ombe na Lumumba jijini ambayo inajihusisha a masuala ya uuzaji na usambazaji wa vifaa mbalimbali vya umeme hapa nchini,mwanzoni mwa wiki hii ilijitokedha kudhamini shindano la Miss East Africa Morogoro ambalo litafanyika tarehe 21 mwezi huu kwenye ukumbi wa Masuka Vilagge mjini humo.Udhamini wa kampuni hiyo ni watatoa vifaa vya muziki (sound ) itakayotumika siku ya shindano pamoja na mambo mengine kadhaa.
Kwa mujibu wa Sigfred Peter amba Master Kif ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo kutoka kampuni ya King Kif Productions ya jijini Dar es Salaam, udhamini wa kampuni hiyo unathamani ya shilingi Milioni Moja .
Aidha, Master Kif aliendelea kufafanua kuwa fomu za warembo wanaotaka kushiriki shindano zina endelea kutolewa katika ofisi za chuo cha Premium Instute of Hotel Management , Masuka Village Hoteli , The Club mjini Morogoro.Sehemu nyingine ni dukani Globel Electronics ,Nyau Traders ,Morogoro Institute of Hotel Catering & Bussiness Management na duka la Malaika njino Morogoro.
Wasahindi watatu watapata fursa ya kushiriki kwenye shindano la taifa la Miss East Africa Tanzania ambalo linaandaliwa na Rena Events Limited litakalofanyika mapema mwezi Oktoba mwaka huu.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ambao hadi sasa wamejitokeza ni Kiu Investment LTD , Iddi Baka Pandisha Fitness Centre , Screen Master na J.R.T Films Productions .Wengine ni Kaka Mie , Datastar Training College , K-P Wear , The Club , The Premium Institute of Hotel Management na mtandao wa www.king kif.blogspot.com

No comments: