Tuesday, 4 August 2009

NEW ZANZIBAR STARS WANAKUJA NA POA PENZI


Kundi maarufu la muziki wa Taarab , New Zanzibar Modern Taarab lenye maskani yake Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam , lipo mbioni kufanya utambulisho bab'kubwa wa albamu yake mpya inayoitwa 'Poa Mapenzi ' yenye nyimbo tano ambazo zimerekodiwa katika studio za Sound Crafters.
Kwa mujibu wa Mla Mali ambaye ndiye mratibu wa kundi hilo , shoo ya kwanza ya utambulisho wa albamu hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Gymkana mjini Zanzibar tarehe 14 mwezi huu ambapo shoo ya pili itafanyika tarehe 15 mwezi huu katika ukumbi wa Travetine Magomeni jijini Dar es Salaam .
Aidha, Mratibu huyo alizidi kufafanua kwa kutaja majina ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo na waimbaji wake kwenye mabano kuwa ni My Sweat Hearty (Sada Nassoro), Mwenye Kusubiri ( Salama Kassim) , Wallah Siumbuki (Shabaha Salum) na Poa Mpenzi inayobeba jina la albamu hiyo ambayo nyimbo zake tatu tayari zinatamba kwenye vituo vya redio.

No comments: