KATIKA kukwepa vinywaji walivyodai kuwa na kilevi, waumini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo maeneo ya Mazimbu mkoani Morogoro, walitumia soda aina ya Coca Cola badala ya Shampeni katika sherehe ya kuwapongeza maharusi waliofunga ndoa Jumapili iliyopita.
Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club mjini hapa, kabla ya Mchungaji Salvatory Daffi, kuifungua soda hiyo iliyokuwa imezungushiwa maua kibao, aliiombea na kumkabidhi mfunguaji ambaye naye aliipitisha kwa maharusi na wazazi wa pande
zote mbili kwa lengo la kuipa baraka.
Baada ya zoezi hilo kukamilika mfunguaji ambaye ni alikuwa katibu wa kamati ya maandalizi ya harusi hiyo, aliitikisa na kuifungua kwa kutumia kifungulia chupa cha kawaida (opena) ambapo ilifoka na kumwagika kama Shampeni.
Alipohojiwa na mwandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, alisema wao kama walokole hawatumii kinywaji chochote kinachoshabihiana na kilevi.
"Tunajua fika kuna Shampeni zisizokuwa na kilevi lakini kwa kuwa ni jamii ya pombe, tumeamua kutovitumia, ndiyo maana unaona tunatumia soda kwenye sherehe zetu,” alisema katibu huyo.
Tukio hilo la Coca Cola linaonyeshwa katika picha zifuatazo:
No comments:
Post a Comment