Thursday, 12 May 2011

DK BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Uingereza wa Masuala ya Kimataifa (Maendeleo), Stephen Obrien, wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika moja ya ukumbi wa mikutano uliopo katika Ukumbi wa Plenary, unapofanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi Masikini Duniani. Mkutano huo unatarajia kumalizika kesho Mei 13. Kushoto ni Msaidizi wa Waziri huyo, Greg Hicks (kulia) ni Balozi mdogo wa Tanzania nchini Italia, Salvator Mbilinyi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Maalim.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ‘UN Women’, Ms. Michelle Bachelet, wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo jana Mei 11, katika ukumbi wa Mkutano wa Plenary unapoendelea mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi Masikini.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akionyeshwa gazeti linalochapishwa nchini Uturuki, lililochapisha habari kuhusu mbuga ya wanyama ya Tanzania, wakati walipokuwa kwenye hafla ya chakula cha jioni jijini Istabul, Uturuki jana
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akizungumza jambo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dr. Sander Gurbuz, wakati walipokuwa katika hafla ya chakula cha jioni walipoalikwa na wenyeji wao jijini Istabul Uturuki jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake wakati alipoalikwa chakula cha jioni jana Mei 11 jijini Istanbul Uturuki. Katikati ni Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki, Ziya Karahan.
Picha ya Pamoja na wenyeji baada ya hafla hiyo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments: