Ilikuwa tarehe 28 mwezi mai usiku pale Movin Pick ambapo uongozi wa kampuni ya African Stars International (ASET) , ulifanya hafla fupi, madhumuni ya hafla hiyo ilikuwa kuwasikilizisha (listening Part) albamu mpya inayoitwa 'Mwana Dar es Salaam' .
Hivyo, muda wa saa tatu usiku hivi , usikilizaji ulianza ambapo kwenye albamu hiyo ya kumi kutoka bendi hii , albamu hii ina jumla ya nyimbo saba tofauti na albamu nyingine tisa za bendi hii ambazo zote zina nyimbo sita .
Majina ya nyimbo hizo kutoka kwenye albamu hii mpya na watunzi wake kwenye mabano ni Sumu ya Mapenzi ( Khalid Chokora) , Mwisho wa Ubaya ni Aibu Saulo John (Faguson) na ‘Nazi Haivunji Jiwe’ ( Thabit Abdul) .
Majina ya nyimbo nyingine ni ‘Rafiki Mbaya ‘ (Roggert Hegga) , Sitopenda Tena ( Saleh Kupaza ) na Mwana Dar es Salaam ya Charles Gabriel (Chalz Baba) ambayo inabeba jina la albamu hiyo.
No comments:
Post a Comment