Ramsey Nouah, akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
STAA wa filamu kutoka nchini Nigeria, Ramsey Tokumbo Nouah, mapema leo alifanyiwa sherehe fupi ya kuagwa na uongozi wa Hoteli ya Paradise ndani ya Ukumbi wa Savannah Lounge Posta jijini Dar es Salaam.
Pati hiyo ilifanyika baada ya kukamilisha shughuli ya kucheza filamu ya Devil Kingdom, iliyoandaliwa na kampuni ya Kanumba The Great Films Production. Akizungumza kwenye hafla hiyo Ramsey, aliwashukuru wote alioshirikiana nao katika filamu hiyo, huku pongezi nyingi akizielekeza kwa Steven Kanumba ambaye ndiye mwenyeji wake aliyemualika kuja hapa nchini.
Mkurugenzi wa Paradise Hotel Justuce Bagumu (kushoto), akibadilishana mawazo na Ramsey (katikati), ndani ya ukumbi huo na Steven Kanumba.
Baadhi ya uongozi wa Paridise Hotel ukiwa kwenye picha ya pamoja na Ramsey Nouah na Kanumba.
Mameneja wa vitengo mbalimbali wa hoteli hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ramsey Nouah.
Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye kwa sasa anafanya vyema ndani ya tasnia ya filamu Bongo Patcho Mwamba (kulia), akiwa kwenye pozi na Ramsey Nouah.
Ramsey Nouah (kulia), akiteta jambo na Mkurugezi wa Paradise Hoteli.
Msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa kwenye pozi na Patcho Mwamba.
Ramsey Nouah, akipozi na Lulu.
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja, akiwa kwenye pozi na Ramsey Nouh.
Steven Kanumba, akipozi na Kajala.
No comments:
Post a Comment