SHINDANO la kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, limewadia ambapo warembo hao wataanza kuchuana rasmi mei 6 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Sun Cirro Club,
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mratibu wa shindano hilo, Maimartha Jesse, alisema kuwa mshindi atakaye patikana kwa mwaka huu atazawadiwa Duka la Vipodozi lenye thamani isiyopungua shilingi milioni tano, (5,000,000/=), ambalo pia litakuwa Wilaya ya Kinondoni.
Maimartha aliongeza kuwa, Duka hilo litalipiwa kodi na leseni ya mwaka mzima bila kuainisha jina la mmiliki maana atakuwa hajafahamika kwea wakati huo.
Warembo hao wanatalajiwa kuingia kambini kuanzia jumanne ijayo kwaajili ya mazoezi, ambayo watajifua chini ya kiongozi wa Wanenguaji wa Bendi hiyo Kassim Mohamed 'Super K'.
No comments:
Post a Comment