
Mh Prof Juma Kapuya akisalimiana na Mzee Ayubu Chamshama wakati wa kupokea miili ya wanamuziki wa Five Star Morden taarab katikati ni mmoja wa waombolezaji.

Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka alikuwepo pia nyuma yake ni Mkurugenzi wa Screen Master Bw Mdoe.

Waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo Dr Emmanuel Nchimbi akihojiwa na vyombo vya habari mbali mbali wakati wa kupokea miili ya marehemu ilipowasili.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani kikiwasili na msafara wa magari uliobeba maiti 12 za wanamuziki wa kundi la Five Modern Taarab waliofariki katika ajali iliyotokea Mikumi mkoan Morogoro,wakati kundi hilo likitokea kwenye ziara ya kimuziki katika mikoa ya kanda za Nyanda za juu kusini.Miili hiyo ilipokelewa kwa pamoja katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ali wilayani Temeke ambako ndiyo yalikuwa makao makuu ya bendi hiyo.Mapokezi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo Dr Emmanuel Nchimbi,Mbunge na waziri wa zamani Prof Juma Kapuya,mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu,Asha Baraka ambaye ni mkurugenzi wa ASET na viongozi wa kundi la muziki wa taarab la TOT na wengine wengi.

Mwili wa marehemu Husna Mapande ukishushwa kwenye gari.

Mwili wa marehemu Issa Kijoti ukishushwa kwenye gari.

Maiti za wasanii hao zikiandaliwa tayari kwa kushushwa kwenye gari na kukabidhi kwa ndugu wa marehemu.

Hapa waombelezaji wakishusha jeneza mara baada ya kuwasili makabaruni.
No comments:
Post a Comment