ashabaraka
Monday, 4 July 2011
Friday, 1 July 2011
Wednesday, 29 June 2011
Monday, 6 June 2011
MISS TABORA HUYU HAPA!
Miss Tabora 2011, Flora Michael (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi wa pili Maua Kimambo (kushoto), na mshindi wa Dalilah Gharib.
MSHINDI wa kwanza kwenye kinyang'anyiro hicho amejinyakulia zawadi ya Dell Laptop yenye thamani ya sh, laki 7,000,00, na kusoma kwenye chuo cha Utalii Msoma ambapo thamani ya masomo hayo ni shilingi laki 3,000,00, huku mshindi wa pili naye akipokea Dell computer ya sh 6,000,00 na Elimu ya Utalii kwenye Chuo cha Tabora. kwa thamani ya sh. 2,000,00 na mshindi wa tatu akiondoka na Subwoofer na dvd player vyenye thamani ya sh. 2500,00 na kuapata elimu ya Utalii kwenye chuo cha Msoma.
Mashindano hayo yalifanyika ndani ya ukumbi wa New Royal Garden mjini hapo huku wasanii wa muziki wa Kizazi kipya Amini H Mbizo, Nash D, Bekah.na Steve R&B wakimwaga burudani pande hizo.
MANDELA NA MIZUKA YA KIGOMA!
Mnenguaji Bakari Kisongo ‘Mandela’, akionyesha "machejo".
Mrembo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, akiwa amepagawa na muziki.
KAMA ilivyo ada, mtandao huu namba moja kwa habari na burudani hapa Bongo, kamera yetu iliingia mzigoni kutafuta mawili-matatu kwa ajili yako wewe msomaji wetu na mfuatiliaji wa habari zetu. Yafuatayo ni baadhi ya matukio hayo Viwanja vya Leaders na Billicanas Club:
Staa wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ na Agness Jerald wakiserebuka.
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Shabani Katwila Q-Chillah (kushoto) na Raheem Rummy Nanj ‘Bob Junior’ wakifuatilia shoo ya Twanga Pepeta jana Jumapili viwanja vya Leaders.
Mnenguaji wa Twanga Pepeta, Abilay Mzungu, akionesha ufundi wake.
Side Boy, mnenguaji wa Twanga Pepeta akiwa kazini.
Msanii wa kizazi kipya, Linnex, akikamua jukwaani Billicanas Club.
Saturday, 28 May 2011
NUSU FAINALI KIMWANA MANYWELE YAFANA
Baadhi ya washiriki wa kinyang’anyiro hicho, wakiwajibika stejini.
HATUA ya nusu fainali ya kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, usiku wa kuamkia leo imefana vilivyo ndani ya Club Sun Cirro Shekilango, Dar es Salaam.
Katika mchujo huo, vimwana 10 wamechaguliwa kuingia fainali inayotarajiwa kufanyika Juni 17, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.
Tukio hilo lilipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na Kundi la Off-Side Trick.
Waimbaji wa Twanga Pepeta wakipamba shindano hilo kwa kuimba.
Msanii wa Kundi la Off-Side Trick, (kushoto), akikamua kwenye shindano hilo sambamba na mnenguaji wao.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka (kushoto) akiwa kwenye pozi na wageni waalikwa.
Mwimbaji mahiri wa Twanga Pepeta, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ ‘akirap’ kwa staili yake.
Asha Baraka (kushoto), akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo, Maimartha Jesse.
Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiwa ‘bize’ na kazi yao.
Mashabiki waliohudhuria shindano hilo wakishuhudia kwa makini.
Mnenguaji wa Twanga Pepeta, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akizungusha nyonga muda mfupi baada ya kuombwa kucheza pamoja na Kundi la Off-Side Trick.
Maimartha (kulia), akimkaribisha Asha Baraka azungumze machache kabla ya washindi kutajwa.
Vimwana Manywele Twanga Pepeta waliofuzu kuingia fainali wakiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya viongozi wa shindano hilo.
Friday, 27 May 2011
MAI & SAJENT WAKILISHANA KEKI!
Ni ka birthday party ka aina yake, kanamuhusu kimwana wa manywele aliyepita Husna Idd maarufu kama Sajent (pichani juu kulia). Leo ametimiza miaka 22 ya kuzaliwa kwake ingawa keki yake imeandikwa 31. kasherehe hako amekafanya jioni hii pale Kinondoni kambi ya mazoezi ya wakata nyonga wa kike wanaowania taji la kimwana wa manywele Twanga pepeta 2011. Katika kasherehe hako, Sajent alilishana keki kistaili na maimatha jesse na swahiba wake Mary hamis na baadhi ya wanamuziki wa Twanga.....
..Sajenti na Mary (kulia) wakilishana keki kistaili..
MCD akipata kipande chake
...ni utamu tu wa keki jamani
....kula mtoto wangu kipande kidogo
...Gitaa Cake.....
Saturday, 14 May 2011
MISS DAR CITY CENTRE 2011/12 APATIKANA
Miss Dar City Centre 2011/12 Alexia William (katikati), akipunga mkono muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo, (kushoto), ni mshindi namba mbili Salah Israel na mshindi namba tatu, Jennifer Kakolaki.
KINYANG’ANYIRO cha kumsaka Mlimbwende wa Kitongoji cha Miss Dar City Centre 2011/12, jana kilifikia tamati ndani ya Ukumbi wa Lamada Hoteli Ilala jijini Dar es Salaam, baada ya Alexia William, kutwaa taji hilo akiwapiga chini washiriki 17 waliokuwa wakiwania taji hilo.
Huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Salah Israel na ya tatu ikitua kwa Jennifer Kakolaki, mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Msitahiki Meya wa Ilala, Jerry Slaa.
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wakionesha Vazi la Ufukweni.
Washiriki wa Miss Tabata 2011/12 wakishuhudia mashindano hayo.
Mwanamuziki wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ (kulia), akifuatilia mpambano huo na Padeshee John Mange.
Dogo Janja akifanya makamuzi kwenye mashindano hayo.
Kundi zima la Tip Top Connection, likiwajibika kwenye shughuli hiyo.
Muandaaji wa shindano hilo Fatuma Abdullah, (kulia), akikatiza ukumbini hapo na Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’.
Muimbaji wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza (kushoto), akiwa kwenye pozi na Rafikiye aliyefahamika kwa jina moja la Daudi kwenye hafla hiyo.
Mshehereshaji wa mashindano hayo, Millard Ayo, akiwa amepozi nyuma ya jukwaa muda mfupi baada ya mshindi kutangazwa.
Meya wa Ilala, Jerry Slaa (kushoto), akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kiasi cha shilingi 1,000,000.
Wanenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ Asha Said ‘Sharapova’ (kushoto), na Liliani Tungaraza ‘Lilian Internet’ wakiwajibika kwenye shughuli hiyo.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo wakifuatilia kwa makini.